Yettufresh

DraftHomepage
DraftHomepage
previous arrow
next arrow

Bidhaa Zetu

Tunafafanua upya ladha ya mkate mweupe katika akili yako. Pindi uonjapo mkate huu hautarudi nyuma tena.

Utamu katika kila kipande unachokula huku ukialikwa kupata kipande kifuatacho.

Ladha ya kipekee? Haswaa, pamoja na protini za ziada kutoka kwenye karanga bora zinazolimwa Tanzania

Mkate mzuri kiafya wenye ladha ya kipekee uliyookwa kwa ajili yako.

Kuhusu sisi

Sisi ni nani

Yettu Fresh ni chapa ya chakula iliyoanzishwa Babati, Tanzania ikitumia rasilimali asilia za ndani ya nchi na teknolojia ya kisasa kukupa bidhaa zenye ladha fresh. Chapa yetu inasimamia ahadi ya fresh, ladha ya kipekee, na uaminifu katika ahadi zetu tuwahakikishia watumiaji wetu ongezeko la ubora wa viwango vya bidhaa za ndani za kila siku. Hivyo, kama unahitaji bidhaa fresh zenye ubora na ladha ya kipekee mikate ya Yettu Fresh ipo kwa ajili yako.

Ahadi yetu

Yettu Fresh ladha iliyozaliwa nyumbani. Kwanini tunasema hivi? Hii ni kwasababu nyumbani ni mahali pekee unapoweza kupata chakula fresh, chenye ladha ya kipekee na kutengenezwa kwa uhakika, na vitu hivi vitatu ndiyo viungo vikuu vinavyounda chapa yetu ya Yettu Fresh.

Inavyotengenezwa

Mikate ya Yettu Fresh ni chapa ya nyumbani, ya mkate fresh na yenye ladha nzuri (ladha iliyozaliwa nyumbani). Mikate yetu inatengenezwa Babati ikitumia rasilimali za ndani pamoja na teknolojia ya kisasa. Yettu Fresh inatengenezwa na kusambazwa kila siku kwani mikate yetu haiongezewi vihifadhi vyovyote. Yettu Fresh inapatikana katika maduka na mini supermarket mbalimbali ndani ya Babati katika ladha tofauti tofauti kama vile mkate mweupe, mkate wa karanga na mkate mtamu. Hivyo kama ni kifungua kinywa cha familia au kitafunwa cha wakati wowote Yettu Fresh inakupatia ladha iliyozaliwa nyumbani.

Wasiliana nasi:
+255 765 931 | babati@yettufresh.co.tz | JOIN THE FOOD FAMILY LIMITED. P.O.BOX 6076
Arusha, Tanzania.